SERIKALI YATANGAZA KUTOA JUMLA YA AJIRA MPYA UALIMU 26, 000 KUANZIA JANUARI 2014.

Naibu waziri wa nchi (TAMISEMI)
anayeshughulikia elimu;Kassimu Majaliwa 
Huu ni mpango endelevu katika kupunguza uhaba wa walimu
 nchini katika shule za msingi na sekondari.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulia elimu, Kassim Majaliwa aliyasema hayo wakati wa kufunga kikao cha siku tatu cha maofisa elimu wa mikoa na halmashauri za wilaya nchini wanaosimamia elimu ya msingi nchini.